KUANZIA JANUARI 2025, VIVUKO VITAKUWA VINASUBIRIA ABIRIA, SEA TAX KUONGEZWA DAR ES SALAAM: BASHUNGWA
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kushirikiana Kampuni ya Azam Marine zinaendelea kuboresha utoaji wa huduma za usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni – Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo kufikia mwezi Januari 2025 vitaongezwa vivuko vidogo (sea tax) kufikia sita (6) ambapo ushirikiano huo utaondoa changamoto kwa wananchi kusubiri vivuko kwa muda mrefu.