MATUMIZI YA MFUMO UFUATILIAJI NA TATHMINI, CHACHU YA MAENDELEO TEMESA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Lazaro Kilahala amewataka washiriki wanaopata Mafunzo ya matumizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa tathmini kuwa walimu wa watumishi wengine ili waweze kuchochea namna sahihi ya ufanyaji kazi bila kusua sua katika majukumu yao