KAMATI YA MIUNDOMBINU YASHAURI UJENZI WA MADARAJA MAENEO YENYE USAFIRI WA VIVUKO
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Wizara ya Ujenzi kufanya usanifu kwenye maeneo yote yenye huduma za usafiri wa Vivuko na kupanga mikakati ya kudumu ya kujenga madaraja katika baadhi ya maeneo ili kupunguza changamoto zinazokabili uendeshaji wa huduma hizo. Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso(Mb) Agosti 20, 2024 jijini Dodoma wakati Kamati ikipokea taarifa ya ukarabati na ujenzi wa vivuko vipya kutoka kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)