KIKAO CHA UHAMASISHAJI JUU YA UCHAMBUZI KUHUSIANA NA KIWANGO CHA KUZINGATIWA KWA USALAMA KATIKA VIVUKO VYA TEMESA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala akifungua kikao cha uhamasishaji juu ya uchambuzi kuhusiana na kiwango cha kuzingatiwa kwa usalama katika vivuko vya TEMESA, kilichoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa TEMESA Makao Makuu, jijini Dodoma Agosti 16. Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kikiwa na lengo la kuleta uelewa wa Pamoja na kusaidia kuzingatia sheria mbalimbali za vivuko kiusalama.