KASEKENYA AZITAKA TEMESA NA TANROADS DODOMA KUJIPANGA KIMKAKATI

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya amezitaka Taasisi za Wakala wa Barabara (TANROADS) na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) mkoani Dodoma kuweka mikakati ya kufanya kazi kitaifa badala ya kufanya kazi kimkoa kama ilivyokuwa awali.