KASEKENYA AWAKUMBUSHA WATUMISHI TEMESA KUTAMBUA DHAMANA WALIYOPEWA
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania kutambua dhamana waliyopewa na Serikali ni kubwa na hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa kuwepo kwa Taasisi hiyo na kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa ili kuleta tija kwa Serikali na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kasekenya ameyasema hayo leo wakati alipohudhuria kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala huo kama mgeni rasmi, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mjini Dodoma.