SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Picha mbalimbali zikionesha watumishi wanawake kutoka Mikoa mbalimbali wanaowakilisha Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani leo Tarehe 8 Machi, 2023. Watumishi hao wameungana na wanawake wengine kote Duniani katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yakiwa na Kauli Mbiu “UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA.”