BILIONI 7.5 KUKARABATI KIVUKO MV. MAGOGONI

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) leo imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5. Mkataba huo umesainiwa leo katika eneo la kivuko cha Magogoni Kigamboni jijini Dar es Salaam kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Lazaro N. Kilahala na mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd.inayotoka Mombasa nchini Kenya na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo, Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb), Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi nchini.