NAIBU KATIBU MKUU UJENZI AKUTANA NA MENEJIMENTI YA TEMESA

Naibu Katibu Mkuu Ujenzi Ludovick Nduhiye leo amefanya kikao kutathmini utendaji kazi wa TEMESA na menejimenti ya Wakala huo ambapo miongoni mwa mambo waliyoyajadili ni pamoja na nafasi, wajibu na majukumu ya Wizara kwa Wakala, maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, utekelezaji wa bajeti na hali ya ufanisi na tija, mawasiliano kati ya Wizara na Wakala kwa masuala ya utawala pamoja na mkakati wa mawasiliano wa TEMESA. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wakala huo uliopo mtaa wa TEMESA mjini Dodoma.