TEMESA YATUNUKIWA CHETI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene leo amewatunuku vyeti Watendaji Wakuu waTaasisi mbalimbali Mkoani Dodoma ikiwemo Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kwa kutambua mchango wao katika uendelezaji wa Makao Makuu ya Nchi kwa kujenga jengo la Ofisi Mkoani Dodoma. Pichani Mhe. Simbachawene akimbakabidhi Mtendaji Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala Cheti hicho mapema leo.