KIKAO CHA MAPITIO YA UTENDAJI KAZI NUSU MWAKA WA FEDHA 2022/2023 NA BAJETI 2023/2024

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania Lazaro Kilahala ameongoza kikao cha Mapitio ya Utendaji kazi wa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023, kikao hicho pia kinatumika kuandaa mipango na bajeti za vituo vya uzalishaji kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024. Kikao hicho kinafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Makao Makuu ya Wakala huo zilizopo Mtaa wa TEMESA eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.