HATIMAYE MV. KAZI YAREJEA RASMI MAGOGONI
Kivuko cha MV. KAZI kimerejea rasmi katika eneo la Magogoni Kigamboni kwa ajili ya kutoa huduma baada ya kukamilika kwa ukarabati wake mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.4. Kivuko hicho kiliondolewa kwenye maji baada ya kufikia muda wake wa ukarabati mkubwa na kuanza rasmi kukarabatiwa mwezi Juni mwaka 2022 na mkandarasi Songoro Marine Transport Boatyard katika Yadi yake iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.