​SERIKALI YAIKABIDHI TEMESA VIFAA VYA SHILINGI MILIONI 545.8

Serikali imenunua vifaa vya Umeme na Viyoyozi vyenye thamani ya shilingi milioni 545.8 na kukabidhi kwa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kwa lengo la kuboresha utendaji kazi. Akikabidhi vifaa hivyo kwa TEMESA Tarehe 17 Disemba 2022, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Adelard Kweka, alisema hizo ni jitihada za Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuboresha utendaji kazi wa Wakala huo.