SERIKALI YATENGA BILIONI 22.9 KUKARABATI VIVUKO NCHINI

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 22.9 kwa ajili ya kuvifanyia ukarabati mkubwa vivuko 14 na kukarabati miundombinu ya vivuko katika maeneo 11 hapa nchini kwa gharama ya Tshs bilioni 4.1.