WAKURUGENZI WATOA NASAHA KWA WATUMISHI TEMESA DAR ES SALAAM

Mkurungezi wa Huduma Saidizi Bi. Josephine Matiro na Mkurugenzi wa Matengenezo na Huduma za Ufundi Mhandisi Hassan Karonda kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) leo kwa pamoja wamefanya ziara ya kiutendaji kupokea na kusikiliza maoni, changamoto na ushauri kutoka kwa watumishi wa TEMESA Mkoa wa Dar es Salaam.