MTENDAJI MKUU TEMESA AHITIMISHA ZIARA YAKE KIVUKONI MAFIA

Lazaro Kilahala, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) pamoja na timu yake, Tarehe 11 Novemba 2022, wamehitimisha ziara yao ya kiutendaji Mkoani Pwani katika kivuko cha MV.KILINDONI kinachotoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.