MTENDAJI MKUU TEMESA AAGIZA WATUMISHI TEMESA LINDI KUFUATA MIONGOZO

Timu ya viongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ikiongozwa na Mtendaji Mkuu Lazaro Kilahala imeendelea na ziara ya kutembelea Ofisi zake kujionea hali halisi na utendaji kazi unavoendelea kwa kutembelea Mkoa wa Lindi, akiwa Mkoani humo, amezungumza na watumishi na kuwakumbusha kufuata miongozo iliyotengenezwa ili kurahisisha na kuleta ufanisi katika kazi kwakuwa miongozo hiyo ndiyo inayopaswa kuwaongoza katika utendaji kazi wao wa kila siku huku akiwasisitizia kubadilisha mitazamo ya namna wanavyofanya kazi ili kuongeza tija na ufanisi.