ZIARA YA MTENDAJI MKUU YAKAMILIKA SINGIDA

Mtendaji Mkuu TEMESA Lazaro Kilahala akamilisha ziara yake ya kiutendaji Mkoani Singida na kuwapongeza kwa kufikia lengo kipindi cha robo ya kwanza kuanzia Julai mwaka huu huku akiwasisitizia kuendeleza utamaduni wa kujifunza kutoka karakana zingine. Mapema Jana, alifanya ziara katika karakana ya Wilaya ya Kahama na baadae kumtembelea Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba ambapo alimueleza mikakati ya Wakala huo ikiwemo kusimamia miradi ya kusimika mifumo ya Umeme, TEHAMA, Viyoyozi na Elektroniki katika majengo mapya yanayotarajiwa kuanza kujengwa katika manispaa hiyo hivi karibuni kabla yakutembelea karakana ya Mkoa Tabora ambapo pia alizungumza na watumishi wa karakana ya Mkoa huo na kuwaagiza kujelekeza kwenye kuzalisha zaidi, kukusanya zaidi na kumridhisha mteja.