​KILAHALA AENDELEA NA ZIARA, LEO NI SIMIYU & SHINYANGA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania Lazaro N. Kilahala leo ameendelea na ziara yake ya kiutendaji ambapo amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ili kupata mrejesho, maoni na changamoto wanazokutana nazo, namna wanavyopokea huduma wanazopatiwa na ofisi za Wakala huo katika Mikoa yao na nini wanatamani kiboreshwe ili kuimarisha huduma za TEMESA katika Mikoa husika.