MIKATABA YA BILIONI 60.3 YA UJENZI NA UKARABATI WA VIVUKO YASAINIWA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imesaini mikataba yenye thamani ya shilingi bilioni 60.3 kwa ajili ya ujenzi wa vivuko vipya, ukarabati wa vivuko vinavyoendelea kutoa huduma ambavyo muda wake wa ukarabati umefikia pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vivuko kote nchini. Hayo yamebainishwa leo wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa msingi (Keel Laying) wa ujenzi wa kivuko kipya kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Kisorya Wilayani Bunda Mkoani Mara na Rugezi Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza, hafla iliyofanyika katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza.