WAZIRI MBARAWA AMTAKA MKANDARASI SONGORO KUMALIZA UKARABATI MV KAZI KWA HARAKA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa amemataka mkandarasi Songoro Marine Boatyard kuhakikisha anamaliza haraka ukarabati anaoufanya kwenye kivuko cha MV. KAZI ili kiweze kurejea haraka kutoa huduma katika kivuko cha Magogoni Kigamboni jijini Dar es Salaam. Profesa Mbarawa ametoa maagizo hayo mapema leo wakati alipotembelea eneo la Yadi ya Songoro Kigamboni Jijini Dar es Salaam kukagua maendeleo ya ukarabati wa kivuko hicho ambacho kwa mujibu wa mkandarasi kinatakiwa kurejea kutoa huduma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.