KIKOSI CHA UMEME KINATEKELEZA MRADI WA BILIONI 12 MJI WA SERIKALI MTUMBA

Ofisi ya Kikosi cha Umeme Kanda ya Kati Dodoma inasimamia mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 12 wa kusimika mifumo ya Umeme, Elektroniki, TEHAMA, Viyoyozi, Lifti, Kangavuke pamoja na kamera za usalama katika mji wa Serikali Mtumba mjini Dodoma. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kikosi cha Umeme Kanda ya Kati Dodoma Mhandisi Deogratius Tarimo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo. Mhandisi Tarimo amesema mradi huo unahusisha jengo la Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambapo Kikosi cha Umeme kinasimika mifumo ya Umeme, TEHAMA, Lifti na Viyoyozi. Mradi huo kwa jengo hilo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.1.