TEMESA NDANI YA MAONESHO YA KIMATAIFA SABASABA

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) unashiriki katika Maonesho ya 46 Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. Wakala unawakaribisha wananchi wote wanaotembelea Maonesho hayo kufika katika Banda la Wakala lilipo ndani ya Holi la Jakaya Kikwete banda nambari 51 kwa ajili ya kujifunza na kupatiwa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na Wakala ikiwemo huduma za vivuko ambapo wananchi watapata nafasi ya kufundishwa namna ya kujiokoa pindi inapotokea dharua ndani ya kivuko, namna ya kuvaa boya la kujiokolea, namna ya kutumia maboya makubwa ya kujiokolea na jinsi ya kutumia kwa usahihi vivuko pamoja na vifaa hivyo vya uokozi. Vile vile mwananchi utapata kupewa elimu kuhusu namna ya kutambua na kutofauitisha vipuri feki na halisi vya magari, utapewa ushauri wa kitaalamu kuhusu Umeme na Elektroniki katika majumba, viwanda na taasisi pamoja na kupewa elimu kuhusu matumizi ya taa za barabarani ambazo Wakala pia unazisimamia. SABASABA 2022 ''Tanzania mahali sahihi pa biashara na uwekezaji''