TEMESA WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI

Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) wamepatiwa mafunzo ya Uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi nchini. Mafunzo hayo yaliyochukua siku mbili yamehusisha mameneja wa Mikoa, wakuu wa vituo, wakuu wa vivuko na karakana, wakuu wa Idara na vitengo, wakurugenzi pamoja na Mtendaji Mkuu. Mafunzo hayo ya Uongozi yamefanyika katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya Wakala huo ,mtaa wa Tambukareli mjini Dodoma.