TEMESA YASHIRIKI SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI

Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kote nchini leo Mei , 01, 2022, wameungana na wafanyakazi wengine kote Duniani katika kusherehekea siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi kwa kushiriki maandamano ambayo yamefanyika katika Mikoa mbalimbali kote nchini. Wafanyakazi hao wameshiriki katika kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango unaofanywa na watumishi wa Wakala huo katika kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inaendelea kufanyika kwa ufanisi. Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yakiwa na Kauli mbiu, ''Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ndio kilio chetu, kazi Iendelee'', kitaifa yamefanyika Mjini Dodoma ambapo Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo leo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.