MTENDAJI MKUU AWAAGIZA WATUMISHI TEMESA KUBUNI NAMNA BORA YA KUMRIDHISHA MTEJA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala amewaagiza watumishi wa Wakala huo kuhakikisha wanawajibika katika kupata mrejesho wa huduma wanazotoa kutoka kwa wateja wanaowahudumia ili kutafuta namna bora ya kuwaridhisha wateja hao.