KIKOSI CHA UMEME KINASHIRIKI MRADI WA USIMIKAJI UMEME JENGO LA UTUMISHI DODOMA

Wataalamu kutoka Kikosi cha Umeme TEMESA Dar es Salaam wanashiriki zoezi la kusimika mifumo ya Umeme katika mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali (Magufuli City) mjini Dodoma.