MKUU WA WILAYA YA ILALA AIPONGEZA TEMESA DAR ES SALAAM KWA HUDUMA NZURI

''Kwenye utumishi wangu kwa Umma, kwa mara ya kwanza naweza nikashuhudia kikao hiki muhimu cha kati ya TEMESA na wadau wake anaowapa huduma, hongereni sana TEMESA, hii inaonyesha ni namna gani mmejipanga kuhakikisha kwamba mnaboresha huduma zenu lakini wateja wenu wanapata maboresho ambayo mnayafanya ndani ya Taasisi ili na wao waweze kujua ni mambo gani ambayo yalikuwa yanawasibu na sasa yamepatiwa majawabu, lakini niwashukuru pia nyinyi wadau kwa upande mmoja, bila nyinyi mkutano huu usingefanyika'' Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati akifungua Kikao cha Pili cha Wadau kufanya tathmini ya mikakati ambayo iliwekwa katika kikao cha kwanza ambapo pamoja na hayo kikao hicho pia kiliweza kusikiliza changamoto maoni na ushauri kutoka kwa wadau wanaotumia huduma za Wakala huo katika Mkoa wa Dar Es Salaam. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Lamada uliopo Ilala jijini Dare Es Salaam.