KAMATI YA BUNGE YAISHAURI TEMESA KUJIENDESHA KIBIASHARA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mheshimiwa Seleman Kakoso (Mb), amewaongoza wajumbe wa kamati hiyo, kukagua miradi ya ukarabati wa karakana na vivuko inayosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jijini Mwanza na kuushauri Wakala huo kujiendesha kibiashara. Kamati hiyo imekagua mradi wa ukarabati wa Karakana ya TEMESA mkoa wa Mwanza unaogharimu Shilingi Milioni 500 ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu, ambapo hadi sasa tayari Mkandarasi wa mradi huo ameshalipwa kiasi cha shilingi Milioni 300.