WANAWAKE TEMESA WASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI CHEMBA

Leo tarehe 8 Machi, 2022 Wanawake Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme kote nchini wameungana na wanawake wengine Duniani katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani. Katika Mkoa wa Dodoma, maadhimimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, yakiwa na *Kaulimbiu ya ''Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu'' Tujitokeze Kuhesabiwa. Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka.

Tanzania Census 2022