TEMESA DAR ES SALAAM YAFANYA ZIARA YA KIMAFUNZO ZANZIBAR
Watumishi wa TEMESA Dar es Salaam karakana ya Vingunguti wamefanya ziara ya kimafunzo na Kubadilishana uzoefu na wenzao wa Zanzibar. Ziara hiyo ya kubadilishana uzoefu iliratibiwa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar wakishirikiana na Wakala wa Karakana Kuu ya Magari Zanzibar. Wakiwa mjini Unguja, watumishi hao wamepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe. Amour Hamil Bakari katika ofisi zake zilizoko mtaa wa Kisauni mjini Zanzibar. Ziara hiyo iliendelea tena siku ya Jumamosi amapo watumishi hao walipata fursa ya kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea Mbuga ya Hifadhi ya Jozani Chwaka Bay. Ziara hiyo iliyochukua siku tatu imehusisha pia mpira wa miguu ambapo timu ya TEMESA ilifanikiwa kuifunga timu ya Wizara ya Ujenzi Zanzibar kwa magoli manne kwa matatu.