TEMESA YAOMBA RADHI KUFUATIA KUSIMAMA KUTOA HUDUMA KWA MV.KAZI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala leo ametembelea na kukagua Kivuko cha MV Kazi ambacho kilishindwa kutoa huduma kwa siku nzima ya jana kufuatia kupata hitilafu ambayo ilitokea majira ya asubuhi. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua Kivuko hicho, Mtendaji Mkuu Kilahala amesema kulitokea hitilafu ambayo ilisababisha kusimama kwa kivuko hicho ili kiweze kufanyiwa marekebisho ambayo yalichukua siku nzima kukamilika na hivyo kusababisha adha kubwa kwa abiria ambao wanategemea kivuko hicho.