‘’MIPANGO SAHIHI YA TAASISI NDIYO ITAFANIKISHA TUFANIKIWE’’ MTENDAJI MKUU TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala amewaagiza mameneja na wakuu wa vituo vya Wakala huo kuhakikisha wanakuwa na mipango sahihi ya kitaasisi ambayo itawezesha TEMESA kuwa na mafanikio kwa kupanga mipango sahihi na kwa wakati huku wakihakikisha inatekelezeka na inaleta tija ambayo imekusidiwa.