TEMESA YATOA MSAADA WA VITI 5 KWA WATU WENYE ULEMAVU KUPUNGUZA KERO YA USAFIRI
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wamekabidhi viti vitano vya watu wenye ulemavu kwa asasi za haki na Usawa kwa Watu wenye Ulemavu ili viweze kusaidia kupunguza changamoto za usafiri kwa watu hao. Akizungumza katika zoezi hilo lililofanyika katika ofisi ndogo za TEMESA leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Meneja wa Vivuko vya Magogoni Kigamboni Mhandisi Samwel Chibwana amesema wamekuwa wakiendelea kushirikiana na jamii kuwapa misaada pale bajeti ikiwa inaruhusu kwa mujibu wa mgawio kwa kuwahudumia wale wenye ulemavu katika jamii.