MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA UZALISHAJI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala amewataka watumishi wa Wakala huo kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza uzalishaji na kuongeza pato la Wakala huo. Mtendaji Mkuu ametoa maaagizo hayo wakati wa ziara yake kiutendaji aliyoifanya mwanzoni mwa wiki hii katika Mikoa ya Mwanza, Geita na Mara ambapo ametembelea karakana za mikoa hiyo pamoja na vivuko ambavyo vinatoa huduma katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.

Tanzania Census 2022