MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA UFANISI KATIKA UTENDAJIKAZI
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala leo amefanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika vituo vya Wakala huo viliyopo jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni sehemu ya kujionea shughuli za vituo hivyo zinavyoendelea na pia kufahamu vizuri Wakala huo, kujifunza na kuuelewa Wakala zaidi.