KIKOSI CHA UMEME KINASHIRIKI KUSIMIKA MIFUMO YA UMEME KIWANDA KIPYA MSD

Wakala wa Ufundi na Umeme kupitia Kikosi cha Umeme unaendelea na kazi ya kusimika mifumo ya Umeme katika kiwanda kipya cha Bohari ya Madawa nchini MSD kinachojengwa Wilayani Makambako Mkoani Njombe katika eneo la Idofi. Akizunguma wakati akikagua maendeleo ya mradi huo, Meneja wa Kikosi cha Umeme nchini Mhandisi Pongeza Semakuwa amesema kiwanda hicho kinachojengwa kitakua maalumu kwa ajili ya utengenezaji wa dawa na (gloves) maalumu kwa ajili ya kufanyia upasuaji. Amesema mradi huo unatekelezwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD), "Mradi huu umehusisha usimikaji wa mifumo ya umeme kuanzia kwenye transfoma mpaka ndani'', ameongeza kuwa tayari kikosi chake kimeshamaliza kazi ya kuwasha umeme huo na kwa sasa wanamalizia kusimika mifumo mingine iliyobakia.