KIKOSI CHA UMEME MABINGWA BONANZA MBEYA
Timu ya Kikosi cha Umeme leo imetwaa ubingwa katika Bonanza la michezo ambalo limeshirikisha ofisi za Wakala huo kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Iringa,Ruvuma, Vingunguti Dar es Salaam, TEMESA Magogoni, Kikosi cha Umeme Dar es salaam, Dodoma pamoja na Njombe.Timu hiyo imefanikiwa kuifunga timu ya TEMESA Dodoma kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo huo kumalizika kwa bao moja kwa moja ndani ya dakika tisini za mchezo. Bonanza hilo ambalo limefanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Meta Mkoani Mbeya limeshirikisha taasisi mbali mbali zilizoko Mkoani Mbeya ikiwemo Chuo cha Uhasibu TIA, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Gereji ya Highland motors pamoja na Mtoni Gereji. Akizungumza wakati wa kufungua Bonanza hilo Eng. Adelard Kweka Mkurugenzi wa Uendeshaji Vivuko ambaye amemuwakilisha Mtendaji Mkuu amewataka watumishi hao kua na umoja katika kazi na kuwapongeza TEMES Mbeya kwa kuandaa bonanza hilo kwani limeleta taasisi hizo pamoja na kujenga ukaribu baina ya taasisi hizo. Timu ya Kikosi cha Umeme imeshinda kikombe, mbuzi pamoja na mpira kama zawadi za mshindi wa kwanza.