MWENYEKITI BODI YA USHAURI TEMESA ATEMBELEA KARAKANA YA MKOA MBEYA
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Profesa Idrissa Mshoro ametembelea na kukagua karakana ya Mkoa wa Mbeya iliyofanyiwa ukarabati mkubwa mapema leo na kuitaka ianze kuonyesha mwelekeo mzuri kwa kukusanya mapato zaidi, Vile vile Profesa Mshoro alipata wasaa wa kukagua karakana ya mitambo ya TEPU ambapo ameipongeza karakana hiyo kwa kuendelea kufanya kazi nzuri ya kufufua mitambo, aidha ameahidi kuisaidia karakana hiyo ili iweze kuongeza idadi ya mitambo inayoisimamia.