SERIKALI YATOA BILIONI 6.3 KUKARABATI VIVUKO NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa ajili ya kuvifanyia ukarabati mkubwa vivuko nchini ambavyo vimefikia muda wake wa ukarabati. Hayo yamebainishwa leo wakati wa mapokezi ya kivuko cha MV. MAFANIKIO kilichorejea kutoa huduma Mkoani Mtwara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake uliochukua takribani miezi miwili na nusu.