BILIONI 2.9 ZAKARABATI VIVUKO VYA MV. SENGEREMA NA MV. TEGEMEO

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) imekamilisha mradi wa ukarabati wa vivuko viwili vinavyotoa huduma Mkoani Mwanza kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.9. Vivuko hivyo, MV. SENGEREMA kinachotoa huduma kati ya Kigongo Wilayani Misungwi na Busisi Wilayani Sengerema na MV. TEGEMEO kinachotoa huduma kati ya Kaunda Maisome na Kanoni Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema, vimefanyiwa ukarabati mkubwa baada ya kufikia muda wake wa kufanyiwa ukarabati ambayo imekuwa ni desturi inayofanywa na Wakala huo mara kwa mara ili kuhakikisha vivuko hivyo vinaendelea kutoa huduma bora wakati wote vikiwa katika hali ya usalama.