CHAMURIHO AITAKA TEMESA KUONGEZA KARAKANA ZA WILAYA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho ametoa wito kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuongeza idadi ya karakana za wilaya katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kusogeza zaidi huduma hiyo kwa maeneo ambayo yako mbali na karakana za Mikoa na Wilaya. Dkt. Chamuriho ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika mkutano wa Baraza la wafanyakazi la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao makuu mjini Dodoma, amesema mkutano huo ni mahususi na muhimu kwani una lengo la kuboresha utendaji kazi na kushirikisha watumishi kwenye maamuzi ili kufikia lengo la kuongeza ufanisi na tija kwa Wakala.