TANGAZO KUHUSU MFUMO WA KUTUMIA KADI KIVUKO CHA MAGOGONI KIGAMBONI

Imewekwa Tuesday 8th Feb , 2022

TEMESA inapenda kuwakumbusha abiria wote wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni kwamba mwisho wa matumizi ya tiketi za karatasi kwenye kivuko cha Magogoni Kigamboni ni Tarehe 28 Februari 2022. Abiria wote mnaombwa kuzingatia agizo hilo ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza. Kadi za N-CARD zinapatikana pande zote mbili za kivuko kupitia kwa mawakala wa N-CARD na wafanyakazi wa Kituo cha National Internet Data Center waliopo maeneo hayo ya kivuko.

Kwa msaada zaidi wa jinsi ya kupata kadi hizo na jinsi ya kuweka salio tafadhali katika ofisi zetu zilizopo upande wa Magogoni au waone wataalamu kutoka NIDC au tupigia kwa namba hii 0800110379.