MAFANIKIO YA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA TEMESA
Imewekwa Thursday 14th Nov , 2019
MAFANIKIO YA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA).
1.0UTANGULIZI
Wakala wa Ufundi na Umeme (The Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency (TEMESA) ulianzishwa chini ya Sheria ya Wakala Na. 30 ya mwaka 1997 na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 254 la tarehe 26 Agosti, 2005. Wakala ulizinduliwa rasmi na Serikali tarehe 23 Juni, 2006.TEMESA ilikasimishwa karibu majukumu yote yaliyokuwa yanatekelezwa na Idara ya Ufundi na Umeme chini ya Wizara ya Miundombinu kwa malengo ya kutoa huduma bora na kwa ufanisi katika Nyanja za Uhandisi Mitambo, Umeme,Elektroniki na Uendeshaji wa Vivuko.
Dira
Kuwa Taasisi yenye ufanisi na ubunifu inayotoa huduma za kihandisi Tanzania bara kwa ajili ya kumridhisha mteja ifikapo 2021.
Dhima
Kutoa huduma za uhakika,salama na zenye ubora wa hali ya juu katika fani ya uhandisi mitambo, umeme na elektroniki, huduma za vivuko na ukodishaji mitambo kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
2.0MAJUKUMU YA TEMESA
Majukumu ya msingi ya TEMESA ni pamoja na kufanya matengenezo ya Magari, pikipiki na Mitambo ya Serikali katika Karakana ambazo zipo kila Mkoa, Kufanya matengenezo, usanifu na usimikaji wa Mifumo ya Umeme, Mabarafu,viyoyozi naelektroniki, Kukodisha mitambo na magari kwa ajili ya usafiri wa Viongozi (VIP Vehicles),Uendeshaji wa Vivuko vya Serikali,pamoja na Kutoa ushauri wa Kitaalamu kwa Serikali na Umma kwa ujumla katika nyanja zauhandisi wa Mitambo, Umeme na Elektroniki.
Hadi mwezi Novemba, 2019 Wakala ulikuwa na jumla ya Watumishi 1,044. Kati ya hao wakudumu ni 587 na mkataba ni 457.Watumishi wakudumu wanajumuisha wahandisi 79, Mafundi sanifu 282 na 223 ni kada zingine. Aidha watumishi wengi wa mikataba wanafanya kazi katika uendeshaji wa vivuko hasa katika kukusanya mapato.
3.0MAFANIKIO YA TEMESA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO TANGU 2015/16 HADI 2019/20
3.1HUDUMA ZA VIVUKO
Wakala umeendelea kuboresha na kusimamia uendeshaji wa Vivuko vya Serikali nchini kwa kuendelea kuongeza idadi ya Vivuko kutoka kumi na tatu (13) wakati Wakala unaanzishwa mwaka 2005 hadi kufikia thelathini (30) katika vituo 19 Tanzania bara pamoja na boti ndogo tano. Hili ni ongezeko la Vivuko kumi na saba (17) sawa na ongezeko la takribani asilimia 131%. Kwa sasa TEMESA inatekeleza mpango mkakati wake wa tatu tangu kuanzishwa kwake ambao umeanza 2016/17 na utaishia 2020/21. Katika mpango mkakati huu:
3.2UNUNUZI WA VIVUKO VIPYA
Wakala umefanikiwa kufanya ununuzi ya vivuko vitatu ambavyo ni MV KAZI kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni mkoani Dar es Salaam ambacho kimegharimu shilingi bilioni 7.3, MV MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza ambacho kimegharimu shilingi bilioni 8.9, MV TANGA kinachotoa huduma kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga ambacho kimegharimu shilingi bilioni 4.02, Ujenzi wa vivuko vyote hivyo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 20.22.
Ununuzi wa boti ndogo tano (5), ambazo ni, MV TANGAZO kinachotoa huduma ya dharura kati ya Kilambo na Namoto mkoani Mtwara, MV KUCHELE kinachotoa huduma ya dharura kati ya Msangamkuu na Msemo mkoa wa Mtwara, MV MKONGO kinachotoa huduma kati ya Utete na Mkongo mkoa wa Pwani, MV BWENI kinachotoa huduma ya dharura kati ya Pangani na Bweni mkoa wa Tanga pamoja na MV SAR III. Ujenzi wa boti hizo zote umegharimu kiasi cha shilingi milioni 415.
- 3.3 UJENZI WA VIVUKO VIPYA UNAOENDELEA
Wakala kwa sasa inatekeleza ujenzi wa vivuko vipya kwa ajili ya maeneo ya, Mafia-Nyamisati ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.3, Bugorola-Ukara ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.2, Chato-Nkome ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.1 na Kayenze-Bezi ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.7. Ujenzi wa vivuko vyote hivi unagharimu jumla ya shilingi za kitanzania shilingi bilioni 15.3
- 3.4UKARABATI WA VIVUKO;
Vivuko vilivyokamilika kukarabatiwa ni pamoja na MV Pangani II na MV Utete. Vivuko vingine ambavyo vinaendelea na ukarabati kwa sasa ni MV Kigamboni, MV Sengerema na MV Misungwi. Aidha Serikali imekua ikiendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa vivuko vingine kwa ajili ya kuboresha huduma ya vivuko ambapo kwa mwaka huu wa fedha imekwishatoa kisi cha shilingi bilioni 2.4. Vivuko vinavyotarajiwa kuanza kukarabatiwa nipamoja na MV Ilagala, MV Kome, MV Musoma,MV Kilombero II, MV Ujenzi, MV Tegemeo,MV Mara,MV KIU na MV Kilombero I.
Wakala pia umefanikiwa kufanya ujenzi wa maegesho mapya kwa ajili ya kivuko cha Kayenze na Bezi na Mlimba Malinyi ambapo gharama za mradi ili kukamilisha ujenzi wa maegesho hayo ni shilingi bilioni 1.9
- 3.5UBORESHAJI WA USALAMA NA MAZINGIRA YA VIVUKO
Mambo ya msingi yanayofanywa hapa ni pamoja na, kutoa elimu kwa watumiaji wa vivuko kabla ya kivuko kuanza safari. Elimu hii hujumuisha jinsi ya kutumia kivuko pamoja na vifaa vya kujiokolea endapo kutatokea tatizo kikiwa ndani ya maji, kufanya matengenezo kinga kwa vivuko mara kwa mara, kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi wa vivuko kuhusu jinsi yakutumia vivuko, usimamiaji wa huduma ya vivuko, kutoa elimu ya matumizi ya vivuko kwa abiria, kufunga vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha usalama katika maeneo ya vivukozikiwemo “CCTV cameras”, pamoja na kuongeza vifaa vya kujiokolea kama life Jackets, life rafts na life rings)pamoja na kuandaa Mfumo wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Mienendo ya Vivuko kwa kudhibiti uzito wa abiria na mizigo inayobebwa kwenye vivuko. (FerryManagement System).
3.6UBORESHAJI WA KARAKANA
Hadi sasa wakala una idadi ya karakana 26 katika mikoa yote Tanzania na karakana 1 katika ngazi ya wilaya ambayo ipo Wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro lengo likiwa ni kusogeza huduma kwa wateja wa Wilaya za Mrimba, Malinyi na Ifakara ambao wako mbali na karakana ya mkoa wa Morogoro.
i.Wakala umeanzisha Mobile Workshop Track, karakana hii inayotembea imegharimu jumla ya shilingi milioni 95 na itakua ikitoa huduma mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuhudumia kwa makundi magari ya Bohari ya Dawa (MSD) yapatayo 100, kutoa huduma mkoa wa Pwani katika Wilaya za Bagamoyo, Utete, Mkuranga pamoja na Kisarawe, vilevile karakana hiyo inayotembea itahudumu iwapo kutatokea dharura kwa magari ya Umma maeneo ya barabara ya Morogoro.
ii.Karakana pia zimefungwa CCTV cameras kwa ajili ya kuimarisha usalama.
iii.Hata hivyo Wakala tayari uko katika mpango wa kusogeza huduma za karakana katika Wilaya ambazo ziko mbali na makao makuu ya mikoa. Wilaya hizo ni pamoja na; Kahama,Same na Simanjiro
iv.Wakala umeanzisha ununuzi wa vipuri kwa wingi (Bulk Procurement of spare parts) ili kupunguza gharama za matengenezo kwenye karakana zake pamoja na kudhibiti uingizaji wa vipuri bandia.
v.Wakala pia umenunua vitendea kazi vya karakana vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni 260 ambavyo kwa kuanzia tayari vimeanza kusambazwakatika karakana zake 12 zilizo Katavi, Geita, Songwe, Pwani, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Rukwa, Morogoro, Kahama, Ifakara, Singida na Lindi.
3.7UKARABATI WA KARAKANA ZA SERIKALI ZINAZO SIMAMIWA NA TEMESA
Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano Wakala umeweza kukarabati karakana kuuya Mt.Depot pamoja na kufunga vifaa vipya na vya kisasa vya kukagulia na kutengenezea magari. Karakana zingine zilizokarabatiwa ni pamoja na karakana za Singida, Lindi, Dodoma, Mwanza na Ifakara.
Kwakuwa vipuri sasa vinanunuliwa kwa wingi yaani (Bulk Procurement), gharama ya vipuri kwenye karakana za TEMESA sasa ni sawa na zile za kwenye soko, na ili kufanya matengenezo ya magari kuwa na gharama nafuu zaidi tayari tumeanzisha mfumo mpya wa tozo la matengenezo ya magari kwa kuzingatia muda (Man hour rate charging system).
4.0CHANGAMOTO
Wakala unakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea kupunguza kasi katika kutimiza majukumu yake baadhi ya changamoto hizo ni kama ifuatavyo;
i.Madeni makubwa ya Wizara na Taasisi. Wizara na Taasisi za serikali kuchelewa kulipa ankara za huduma zinazotolewa na TEMESA. Changamoto hii hupelekea Wakala kuwa na madeni makubwainayodai kwa wateja hali inayopelekea Wakala kudaiwa na wazabuni wake.
ii.Uendeshaji wa Vivuko ambavyo haviwezi kujiendesha kwa mapato yake. Mapato yanayotokana na uendeshaji wa baadhi ya Vivuko vya Serikali hapa nchini hayatoshelezi kukidhi mahitaji ya uendeshaji wa Vivuko hivyo. Hali hiyo ina ulazimu Wakala kuendelea kutoa huduma katika Vivuko hivyo kwa kutumia fedha kutoka vyanzo vyake vingine vya mapato.
iii.Uchakavu wa miundombinu na vifaa vya Karakana. Miundombinu ya karakana nyingi za TEMESA ni chakavu na haiko katika kiwango cha karakana za kisasa hii inatokana na majengo kujengwa miaka mingi.
iv.Uwasilishwaji wa Fedha za Miradi ya Maendeleo. Pamoja na Serikali kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya Wakala upatikanaji wa fedha hizi umekuwa ni tatizo. Fedha zinazowasilishwa ni kidogo kulinganishwa na fedha zilizoidhinishwa.
v.Uhaba wa Watumishi. Wakala unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi hasa kwenye kada za ufundi katika karakana ya matengenezo ya magari. Tatizo hili linatokana na watumishi wa kada hiyo kufikia umri wa kustaafu pia kibali cha ajira kutotosheleza mahitaji.
MWISHO