MTENDAJI MKUU WA TEMESA ASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA MAFUNDI NA WATEJA
Posted On: October 30, 2026
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Bw. Kheri Mahimbali, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya mafundi na wadau mbalimbali wanaohudumiwa na TEMESA ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma.
Msisitizo huo umetolewa tarehe 26 Oktoba 2026, alipokutana na mafundi wa Wakala kutoka mikoa mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili mafundi katika utekelezaji wa majukumu yao, katika ukumbi wa mikutano wa TEMESA Makao Makuu jijini Dodoma.
Aidha, mafundi wameeleza changamoto zinazowakabili ikiwemo uhitaji wa kuimarisha ujuzi wao katika matumizi ya vifaa vya kisasa vya uchunguzi na utambuzi wa hitilafu pamoja na mbinu mpya za matengenezo na ukarabati ambapo wameeleza kuwa kukabiliana na changamoto hizo kutasaidia kuongeza ufanisi, kupunguza muda wa magari kukaa gereji na kuboresha ubora wa huduma zinazotolewa kwa Serikali na wananchi.