WAZIRI WA UJENZI MH. KADOGOSA APONGEZA USHIRIKIANO WA TAASISI ZILIZOPO CHINI YA WIZARA YA UJENZI
Posted On: October 03, 2026
Waziri wa Ujenzi, Mhe.Masanja K Kadogosa , leo amepokelewa rasmi katika Ofisi za Wizara ya Ujenzi Mtumba jijini Dodoma, kufuatia uteuzi wake na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri wa Ujenzi.
Katika mapokezi hayo, Waziri Kadogosa amepokelewa na Makatibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, akiwemo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA).
Mapokezi hayo yamefanyika ikiwa ni sehemu ya kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Wizara ya Ujenzi, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano, uwajibikaji na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
TEMESA inaendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Ujenzi katika kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma za ufundi, umeme, elektroniki, matengenezo, usimamizi wa vivuko na huduma nyingine za kihandisi, kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha huduma kwa wananchi.