MAHIMBALI AKABIDHIWA OFISI RASMI, AANZA KAZI TEMESA

News Image

Posted On: May 14, 2026

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Bw. Moses Mabamba, tarehe Mei 11, 2026, amemkabidhi rasmi ofisi Bw. Kheri A. Mahimbali aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Wakurugenzi wa Idara mbalimbali pamoja na Menejimenti ya TEMESA na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa TEMESA Makao Makuu, jijini Dodoma. Makabidhiano hayo yanaashiria mwanzo wa ukurasa mpya wa uongozi, uwajibikaji na kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa taasisi za umma na wananchi kwa ujumla.

Inbox