MTENDAJI MKUU TEMESA AKAGUA MAENDELEO YA UKARABATI WA VIVUKO NA UJENZI WA KIVUKO KIPYA
Posted On: October 18, 2026
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Bw. Kheri Mahimbali, amekagua maendeleo ya ukarabati wa vivuko vya MV. KIGAMBONI na MV. PANGANI, ukarabati unaotekelezwa na Kampuni ya Songoro Marine. Aidha, Mtendaji Mkuu amekagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV. KILINDONI II, kinachojengwa na Mkandarasi Dar es Salaam Merchant Group (DMG).
Ziara hiyo imelenga kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo, kujionea hatua zilizofikiwa na kusisitiza umuhimu wa kukamilisha kazi kwa kuzingatia viwango vya ubora na muda uliopangwa, ili kuboresha upatikanaji na ufanisi wa huduma za vivuko kwa wananchi.