WADAU TEMESA MBEYA WANOLEWA MAFUNZO YA MFUMO WA MUM
Wadau wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Mbeya wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Kazi za Matengenezo (MUM), kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya matumizi sahihi ya mfumo huo pamoja na kukusanya maoni kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma zake nchini. Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 22 Mei 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Tughimbe Hotel mkoani humo, yakiendeshwa na Mhandisi Pongeza Semakuwa, Meneja wa Kikosi cha Umeme TEMESA na Mratibu wa Mfumo huo kwa ngazi ya kitaifa ambapo Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wamiliki wa gereji teule pamoja na watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali zinazopokea huduma kutoka TEMESA.