MAAFISA RASILIMALI WATU, WAGAVI NA WAHASIBU TEMESA WAPATIWA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA umeendesha semina maalum kwa wahasibu, wagavi na maafisa rasilimali watu kutoka vituo mbalimbali vya wakala huo. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa TEMESA Makao Makuu na imefunguliwa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala. Akizungumza na watumishi hao wakati akifungua semina hiyo, Mtendaji Mkuu amewataka kuhakikisha kuwa semina hiyo inakuwa chachu ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uwajibikaji, ubunifu sambamba na kuendana na mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanyika ndani ya Wakala.